Episodes

Tuesday Nov 02, 2021
Siku ya Bwana | Mchungaji Moses Waweru | DCIKZ
Tuesday Nov 02, 2021
Tuesday Nov 02, 2021
Siku ya Bwana | Mchungaji Moses Waweru | DCIKZ
Kuna siku tunayoitarajia
2 Wafalme 4:16 Kunayo siku yako ya kutembelewa na Bwana na pia kuna siku ya kurudi Kwa Bwana.
Hii siku imeandaliwa na Bwana na wakati mwingine huwa inaleta hofu.
Isaiah 13:11 Tunatakiwa kujua si eti Mungu anatutega ili atunase au tuanguke na kutuumiza
1 Wathesalonike 5:1-11 1-3 Biblia inasema kuwa Bwana atakuja na tena Kwa ghafla
4-11 Mistari hii inatuhimiza Sisi Kama Wakristo hatufai kuogopa maana hatufai kupatwa kighafla Kwa sababu tunapaswa kuwa imara kila siku.
Angazia silaha za hizi; Vazi la kifuani- inazungumzia kuwa na Imani katika mioyo yetu. Kofia Kama la chuma ambalo ni wokovu, ili tusiwe watu wa giza, tukeshe tukimsubiri Bwana. Hali Ya Maandalizi Kama Bwana Anavyotarajia Waebrania 11:1-3, Yakobo 2:14-16, 1 Wakorintho 13:13 1 Kwa Imani - tuwe watu wa Imani ili tupate kibali kutoka Kwa Mungu. 2. Kwa Upendo - tuwe wavumilivu Kwa kila mmoja na tufanye hivyo Kwa upendo 3. Tumaini - tunahitaji kuwa na tumaini ili tuweze kungoja siku Ile ya Bwana. Safari yetu Kama Wakristo ni Safari ya tumaini. Je tumaini lako liko wapi? Kwa masomo, pesa au maisha yako? Mambo mengine yote yatakwisha lakini haya matatu yatabaki; Imani, Upendo, Tumaini.
#DCIKZ #MountingUp #FeelsLikeHome
No comments yet. Be the first to say something!